2 Corinthians 11:1-5

Paulo Na Mitume Wa Uongo

1 aLaiti mngenivumilia kidogo katika upumbavu wangu! Naam, nivumilieni kidogo. 2 bNinawaonea wivu, wivu wa Kimungu, kwa kuwa mimi niliwaposea mume mmoja, ili niwalete kwa Al-Masihi kama mabikira safi. 3 cLakini nina hofu kuwa, kama vile Hawa alivyodanganywa kwa ujanja wa yule nyoka, mawazo yenu yasije yakapotoshwa, mkauacha unyofu na usafi wa upendo wenu kwa Al-Masihi. 4 dKwa sababu kama mtu akija na kuwahubiria Isa mwingine ambaye si yule tuliyemhubiri, au kama mkipokea roho mwingine ambaye si yule mliyempokea, au Injili tofauti na ile mliyoikubali, ninyi mnaitii kwa urahisi. 5 eLakini sidhani ya kuwa mimi ni dhalili sana kuliko hao “mitume wakuu.”
Copyright information for SwhKC